Changu Chako, Chako Changu

Changu Chako, Chako Changu

Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.

00:00
00:00

Episode's summary

Katika Makala haya, mtangazaji wako Ali Bilali aliezuru Kisumu, amekutana na kufanya mazungumzo na mkurugenzi wa kituo cha utamaduni wa Ufaransa Joshua Kome kuzungumzia historia ya kutuo hicho na mikakati yake kukuza sanaa na utamaduni wa watu kutoka eneo hilo la Kenya. Kumbuka kunifollow @billy bilali

Episodes

314-

Alliance Francaise ya Kisumu, historia yake na mpango wake wa kukuza sanaa.

Katika Makala haya, mtangazaji wako Ali Bilali aliezuru Kisumu, amekutana na kufanya mazungumzo na mkurugenzi wa kituo cha utamaduni wa Ufaransa Joshua Kome kuzungumzia historia ya kutuo hicho na mikakati yake kukuza sanaa na utamaduni wa watu kutoka eneo hilo la Kenya. Kumbuka kunifollow @billy bilali

13 Oct 2026
313-

Changu Chako Chako Changu: picha ya jiji la Kisumu mbali na maandamano oct 4 2026

Katika makala yetu Jumapili hii tunazungumzia kuhusu picha ya mji wa Kisumu tofauti na inavyozoeleka. Alliance Francaise ya Kisumu imeanda mradi unaoulezea mji wa Kisumu kwa aina tofauti. Kila linapotajwa jila la kisumu moja kwa moja unaona maandamano, vurugu, uvuvi, wakati jiji hilo ni mbali kabisa na hayo.

04 Oct 2026
312-

Changu Chako: Historia ya jij la Kisumu septemba 27 2026

27 Sep 2026
311-

Changu Chako: Historia ya ngoma ya utamaduni wa kiturkana Sept 20 20269

Makala haya yanazungumzia kuhusu muziki wa tamaduni ya Kiturkana ambao ni kiungo muhimu sana katika maisha ya jamii ya Waturkana, inayopatikana kaskazini-magharibi mwa Kenya. Muziki wao hautumiwi tu kama burudani, bali ni njia ya kuhifadhi historia, kuwasiliana na jamii, na kuadhimisha matukio muhimu ya maisha. Hapa kuna vipengele muhimu vinavyofafanua muziki wa kitamaduni wa Kiturkana:

20 Sep 2026
310-

Changu Chako: Historia ya watu wa kabila la Wahehe sept 6 2026

Karibu katika makala yetu ya leo Jumapili Changu Chako Chako Changu. Makala haya hukuletea Historia na tamaduni ya makabila mbalimbali, le Parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletza Historia ya watu wa kabila la Wahehe, kutoka chini Tanzania na kwenye Muziki nitakuletea msanii kutoka nchini Uganda Made Ice, Mimi ni Ali Bilali Bienvenue ama Karibu.

06 Sep 2026